Tafuta Elimu Kwanza: Kabla Ya Kutamani Kumiliki Pesa Zaidi.
Umewahi kukaa chini ukajiuliza kwa nini mtu mmoja ana uwezo wa kumiliki pesa nyingi wala hata kuhangaika na mwingine pesa kidogo tu ikiingia mkononi mwake hatulii mpaka hiyo hela itakapokwisha au ikibaki kiasi fulani basi anatulia?
Ninalotaka Silifanyi, Nafanya Nisilotaka!!!
“Umewahi kukutana na mtu halafu akakakuuliza swali hili? “ninalotaka silifanyi,lakini nafanya lile nisilotaka,utanisaidiaje?” hili ni swali ambalo nimekutana nalo mara nyingi nikiulizwa hasa na vijana na leo nimeona niandike hii makala nikiamini kuna namna inaweza kuwa msaada kwa wasomaji wetu wengi”
Jifunze Kupitia Makosa.
Kwa nini watu wengine wananufaika na hali ya kukosea na wengine wanapoteza kabisa mwelekeo wa maisha pale wanapofikia katika hali ya kukosea? Nini kinachofanya watu hao wale tofauti ni nini? Kinachotofautisha watu hao wawili ni namna tofauti katika mitazamo yao,mmoja anaichukia kama fursa na mwingine anaona kama kukosea ndio mwisho wa kila kitu. Ingawa watu wazima wengi wanachukulia kukosea kama njia ya kumsaidia mtu kukua na kupata uzoefu katika maeneo mengi,kinyume chake watu wengi hasa vijana wadogo hawapendi kukosea na hivyo hukatishwa tamaa pale wanapojikuta wamekosea katika maisha.
“Nguvu Ya Imani Katika Kila Unalofanya”
Je, unakumbuka kuwa dunia tunayoishi inaongozwa na kanuni na sheria zilizowekwa? Sheria hizi, kama sheria nyinginezo zilizotungwa na binadamu, zinasimamia mstakabali wa maisha duniani, na zisipofuatwa, wakiukaji hukabiliwa na adhabu.
Safari ya Ndoto: Dr. Kakenya Anayeishi Maono Yake.
Miongoni mwa visa vya kusisimua vya hivi karibuni kutokea katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla ni kisa cha msichana wa kimasai wakati huo ambaye alikubali kukeketwa kwa sharti la kurudi shule baada ya kukeketwa badala ya kuoelewa kama ilivyokuwa desturi ya wamasai. Katika simulizi hii ambayo Kakenya Ntaiya anasimulia mwenyewe utabaini jinsi msichana huyu raia wa Kenya alivyoweza kubadilisha uzoefu na uchungu wa kukeketwa kuwa ndoto kubwa ya kubadilisha maisha ya mabinti wengi wa kimasai.
Huwezi Kuvuna Usichopanda.
Ukipanda machungwa utavuna machungwa, ukipanda mahindi utavuna mahindi. Kile ulichopanda nchicho utakachovuna pia kwa hiyo uwe mwangalifu unapopanda.
Funguo Sahihi kwa Mafanikio
Jioni ilipoingia, nilijikuta nikiwa nimekamilisha majukumu yangu kwa siku hiyo na hivyo kurudi nyumbani mapema kuliko wengine. Kufika nyumbani, nilikuta sikuwa na mtu yeyote, hivyo nilihitaji kufungua mlango mwenyewe kwa kutumia funguo zangu.
Anzia Pale Unapoweza.
Kuna tofauti kati ya kufanya unachoweza kufanya na kufanya unachotaka kufanya. Kufanya unachoweza ni pale unapopaswa kufanya kile kilichopo ndani ya uwezo wako hata kama siyo kama unavyotamani kufanya.Na kufanya unachotaka ni kufanya kile unachotaka bila kuwepo na kizuizi cha aina yoyote.Watu wengi wanaanza kufanya wanachoweza kufanya kabla ya kuanza kufanya wanachotaka.
Kuanzia Ulipo: Njia Kuelekea Kuishi Ndoto Zako.
Umewahi kujiuliza kwa nini mtu mmoja anabaki kulalamika na kushindwa kuanza kuishi ndoto zake kwa kisingizio cha kutokuwa na pesa ya kutosha, wakati huo huo kuna mtu anaanza kuishi ndoto yake kwa kutumia mazingira na pesa kama hiyo hiyo mwenzake anayoita ndogo?
“Unataka Kufanikiwa: Chagua Kipaumbele”
Kama kuna tabia inakwamisha watu wengi kufika katika kilele cha mafanikio wanayostahili duniani,basi ni tabia ya mtu kujaribu kufanya kila kitu katika maisha. Mtu kushindwa kujielekeza katika jambo moja na kujikuta anahangaikia kila fursa inayokuja mbele yake ni kikwazo kikubwa cha watu kufanikiwa.
“Anza Safari: Kuishi Kusudi La Kuwepo Kwako Duniani”
Kila binadamu ameumbwa kuwepo hapa duniani kwa kusudi maalum.Kusudi ndicho kitu pekee kinachomtofautisha mtu mmoja na mwingine pia mchango unaoweza kutoa kipindi cha kuwepo kwako duniani. Kutambua kusudi la kuwepo kwako duniani ni hatua muhimu sana katika maisha kwani ndicho kipimo na kigezo cha mafanikio ya maisha ya mtu na humwezesha mtu kuanza kuishi maisha yake mwenyewe.
“Hamisi: Licha Ya Kutokuwa na Mikono, hategemei mtu”
Japokuwa hana mikono kabisa anaweza kufanya chochote anachotaka kufanya bila kutegemea mtu yeyote yule,anafanya kazi nyingi hata zile ambazo baadhi ya watu wasio na upungufu wa aina yoyote wa viungo hawawezi kufanya. Kwa mfano: kuogelea, kuchunga ng’ombe, kuvua samaki, kulima, kupika,kufyatua matofali, kujenga, kuosha vyombo,kufua,kucheza mpira,kupiga muziki n.k