Huwezi Kuvuna Usichopanda.
Ukipanda machungwa utavuna machungwa, ukipanda mahindi utavuna mahindi. Kile ulichopanda nchicho utakachovuna pia kwa hiyo uwe mwangalifu unapopanda.
Umewahi kusikia ukweli huu kwamba kwa wakati mmoja binadamu anaishi katika aina mbili za ulimwengu? Ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili. Ulimwengu wa mwili ni huu unaoonekana kwa macho ya nyama, na ulimwengu wa roho hauonekani kwa macho haya ya mwili isipokuwa kwa macho ya kiroho.
Japokuwa watu wengi bila kujua wamejikuta wakijielekeza zaidi katika ulimwengu wa mwili, ukweli ni kwamba ulimwengu wa mwili unaendeshwa na ulimwengu wa roho. Mambo yote tunayoona yakitokea na kushuhudia kwa macho chimbuko lake ni kuanzia katika ulimwengu wa roho.
Kama watu wote wangekuwa na uelewa huu basi msisitizo mkubwa ungekuwa kujifunza jinsi ulimwengu wa roho unavyofanya kazi ili kuweza kuuathiri ulimwengu wa mwili. Kama ilivyo katika ulimwengu wa mwili unavyoongozwa na sheria ulimwengu wa kiroho nao unaongozwa na sheria. Wanaojua na kuishi kulingana na sheria hizo wanakula mema ya nchi na wale wanaokiuka sheria za ulimwengu wa roho basi wanahangaika sana kupata matokeo wanayoyataka katika maisha au katika ulimwengu wa mwili.
Ukijua na kuishi kwa kuzingatia misingi ya sheria utafanya chochote unachoamua kufanya bila kukwamishwa na kitu maana umeujua ukweli nao unakuweka mbali na kushindwa sababu unajua ulimwengu wa kiroho na ule wa mwili unavyofanya kazi. Kuna kitu kinaitwa kwa lugha ya kiingereza “The universe laws” kwa kiswahili tunaweza kutafsiri kama “sheria za ulimwengu”. Hizi zinafanya kazi bila kujalisha kama mtu unajua au hujui na matokeo yanaonekana dhahiri katika maisha ya watu.
Umewahi kusikia msemo wa kiswahili “apandacho mtu ndicho atakachovuna” Huu ni memo maarufu sana katika lugea ya kiswahili ambao unafanana sana na kile ninachokwenda kufafanua hapa. Miongoni mwa sheria za ulimwengu ambayo ni maarufu sana katika maisha ya binadamu ni “sheria ya kupanda na kuvuna“. Kile unachopanda ndicho unachotegemea kuvuna.
Mkulima anapopanda mbegu yoyote anategemea kuvuna mazao jamii ya ile mbegu aliyopanda tangu anapopanda. Hawezi mtu kupanda mbegu halafu wakati huo huo anatarajia kutokuvuna atakuwa hajui kile anachopaswa kufanya. Sheria au kanuni hii inasema unachopanda ndicho utakachovuna. Ukipanda mahindi utavuna mahindi, ukipanda mkomamanga utavuna komamanga. Huwezi kupanda mahindi halafu ukavuna maharage badala ya mahindi utakuwa ni muujiza miongoni mwa miujiza kuwahi kutokea maana ni kinyume cha sheria na kanuni ya ulimwengu ya kapanda na kuvuna.
Mambo tunayoona duniani kwa macho ya nyama ni kivuli cha mambo jinsi yalivyo katika ulimwengu wa roho. Hakuna kinachotokea kisichokuwa na chimbuko katika ulimwengu wa roho. Mimi na wewe kwa mfano kwa nje tunaonekana kwa maumbo ya miili yetu lakini ukweli sisi ni roho isiyo na mipaka ambayo inakaa ndani ya hii miili. Mtu wa ndani ndiye anaemarish maili kufanya chochote ambacho ataamua mwili ufanye. Tumeumbwa tukiwa kamili na kila kitu tunachohitaji ili kuwa chochote tunachotaka kuwa katika maisha. Mungu hakuweka upungufu kila kitu tunachohitaji ili kuishi kusudi la kuwepo kwetu duniani ameweka tayari kwa ajili yetu.
Kama ilivyo katika ulimwengu wa mwili tunapanda mbegu katika udongo na asili inasababisha zioze, kuota, kukua na kuzaa mazao tuliyotarajia, ndivyo ilivyo pia katika ulimwengu wa roho. Kuna udogo, mbegu na mbolea ya kufanya mbegu uliyopanda iote, kukua na kukuzalia mazao kama ukivyokusudia. Ukijua siri hii hakuna utakachoshindwa kufanya ukiamua maana imeshaijua siri na kanuni muhimu ya maisha na kuiishi pia.
Kila kitu tunachofanya katika maisha chanzo chake ni katika akili zetu. Kwa mfano huwezi kushinda katika ulimwengu wa mwili kabla hujaamua katika ulimwengu wa roho. Ukichagua kushinda utashinda na ukichagua kushindwa kadhalika utashindwa.Kwa nini? Kwa sababu umepanda mbegu ya kushindwa kwa hiyo huwezi kupokea matunda kinyume. Kumbuka ule msemo “apandacho mtu ndicho atakachovuna” chochote unachopanda katika akili yako kitathibitika katika dunia yako.
Kama ilivyo kwa mkulima akili ndiyo udongo,mawazo ndiyo mbegu ,matendo ndiyo maji na hisia zako ndiyo jua. Endapo utapanda chochote katika akili yako,na kuhisi kana kwamba kimekwishakuwa chako,na kuendelea kutenda kukielekea ni lazima kitathibitika katika maisha yako,kwa sababu ni kanuni.
Ni muhimu sana kujifunza namna akili yetu inavyofanya kazi. Akili ya mwanadamu imegawanyika katika sehemu kuu mbili:conscious mind (akili ya ufahamu) na subconsciuos mind (akili ndogo) hapa kiswahili chake hakijakaa vizuri. Wataalam wa saikolojia wanafafanua kuwa subcosciuus mind ni ile sehemu ya akili ambayo inamsaidia mtu kufanya maamuzi akiwa anatambua kabisa anachofanya. Subconscious mind yenyewe ni sehemu ya akili ambayo inakusanya kila tariff inayosikia,kuona na kutunza.
Sehemu kubwa ya akili ya mwanadamu imetawaliwa na subconsciuos mind kwa zaidi ya 90% na consciuous mind yenyewe inamiliki karibu 10% ya akili yote. subconsciuos mind ni kama kamera ambayo inanasa matukio yote yanayotokea na kuyahifadhi ili yaweze kusaidia kufanya marejeo unapotaka kufanya uamuzi fulani baadaye kwa sababu unao uzoefu fulani. Ubaya wa sehemu hii ya akili haijui kizuri wala kibaya yenyewe inajua kutunza kumbukuimbu tu.
Conscious mind yenyewe ni kama mlinzi anaekaa langoni kuangalia na kuruhusu kile kinachopaswa kuingia na kuzuia kisichotakiwa kisiingie. Ajabu ni kwamba sehemu kubwa ya maisha ya mwanadamu imetawaliwa na subconscious mind.
Katika Biblia kitabu ambacho napenda kurejea katikanyakati tofauti kuna mstari unasema “chunga sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo,kwa maana huko ndiko ziliko chemi chemi za uzima”. KUna uhu siano mkubwa sana wa kufanikiwa au kutokufanikiwa na kile ambacho mtu anapanda katika akili yake. Ukipanda kufanikiwa utafanikiwa na ukipanda kushindwa hakuna mbadala utashindwa kwa sababu ndani mwako umekwisha fanya uamuzi wa kushindwa.
Ndiyo maana tunashauriwa kuwa waangalifu sana ili kuhakikisha kuwa yale ambayo tunayaruhusu ni yale tu ambayo yanatusaidia kuwa watu bora zaidi. Inasisitizwa sana kuwa watu chanya na kuepuka sana mazingira yanayosababisha kuwa katika hali hasi. Watu wanaoona kushindwa tu,wale ambao kazi yao kubwa wao wanaona tu mapungufu kwa watu,walalamishi,wasioridhika na wale wanaoona upungufu tu ni watu wa kuwaepura kwa sababu watasababisha kupanda ndani mwako mbegu ambatyo haitakuzalia matunda ambayo unatarajia. Kuna mstari tena katika Biblia unasema “aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo” hakuna namna utakuwa tofauti na unavyojiona mwenyewe ndani mwako. Watu wengi wanatamani kufanikiwa lakini mioyoni mwao wamekwishafanya uamuzi kushindwa. Ni ngumu.
Unataka kufanikiwa katika eneo lolote la maisha iwe ni biashara,mahusiano,kazi n.k uwe mwangalifu sana kuhakikisha kile unachotaka peker yake ndicho unachopanda ndani mwako maana bila kufanya hivyo utakuja kupata matunda ambayo hukuyategemea.
Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha yako usisite kuwasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo.Tutashukuru kama watakaotutafuta wakiwa ni wale ambao kweli wanaamaanisha.