Tatizo Siyo Fursa

JICHO LA KUONA FURSA

Unawaza nini ndani mwako unapofika mahali umekwama katika mazingira fulani kimaisha? Iwe umefukuzwa kazi uliyokuwa unaitegemea kuendesha maisha,umemaliza shule na unahangaika kutafuta kazi bila mafanikio? Unaona huo kuwa kama mwisho wa kila kitu na milango yote kufungwa au unaona kama ndiyo mwanzo wa milango mingine iliyokuwa haijakufungukia kufungukia sasa?

Karibu tena katika makala zetu za kujenga katika mtandao wa maishanifursa.net Kwanza nikushukru toka ndani ya moyo wangu,kwa kuendelea kutuamini na kufuatilia kazi zetu. Kazi hii ina maana kwa kuwa upo wewe unaefuatialia.Kama ni mara yako ya kwanza kusoma makala zangu nikukaribishe kwa mikono miwili na kuahidi kuwa hutakaa ujute kuufahamu mtandao huu.

Leo kupitia makala hii fupi nataka tutafakari kidogo juu ya mada niliyoipa kichwa “Fursa Siyo Tatizo” Bila shaka ukitafakari vizuri utaona kabisa kichwa cha makala yangu jinsi kilivyo,lipo swali linalotakiwa kujibiwa ndani ya makala hii. Kama fursa siyo tatizo basi tatizo ni nini?

Watu wengi tunatumia na tunalitamka sana neno fursa katika vinywa vyetu.Ukiangalia katika kamusi utagundua neno hili linabainishwa kuwa ni ujumla wa mazingira yanayotengeneza uwezekano wa jambo kufanyika. Kwa lugha ya kiinngereza wanaweka vizuri zaidi, “An opportunity is a set of circumstances that makes it possible to do something”

Unawaza nini ndani mwako unapofika mahali umekwama katika mazingira fulani kimaisha? Iwe umefukuzwa kazi uliyokuwa unaitegemea kuendesha maisha,umemaliza shule na unahangaika kutafuta kazi bila mafanikio? Unaona huo kuwa kama mwisho wa kila kitu na milango yote kufungwa au unaona kama ndiyo mwanzo wa milango mingine iliyokuwa haijakufungukia kufunguka sasa?

Napenda kusikiliza watu kila ninapokwenda,kwa sababu wananipa nafasi ya kujifunza mambo mengi,kwa kuwa kwa kufanya hivyo napata nafasi ya kujifunza sana kupitia mitazamo mbalimbali na namna watu wanavyowaza katika mazingira tofautitofauti na watu wengi wanahangaika sana kutafuta fursa katika maisha.

Kama ambavyo hatujawahi kukatikiwa na hewa inayohitajika kwa ajili ya sisi kuendelea kuwa hai,ndivyo ilivyo hata kwa upande wa fursa zipo nyingi hazina ukomo.Haijawahi,haitokei na haitatokea kuwepo mtu ambaye atafanikiwa kutumia fursa zote zilizopo katika mazingira yake akazimaliza!.

Kwa kujua au hata sisi bila kujua Mungu hajawahi kuacha kutugawia hewa na ndiyo maana unaona maisha yanaenda siku hadi siku. Hebu fikiri siku moja hewa unayovuta ingekuwa ya mgao kama inavyokuwa kwa huduma zetu kama umeme na maji kungekuwa na maafa kiasi gani hapa duniani?

Kila mtu ana uhitaji wa fursa ya namna fulani na changamoto kubwa inayokabili watu wengi ni namna gani ya kuzipata hizo fursa.Watu wanahaha kutafuta fursa na fursa zinahangaika kutafuta watu wanaotafuta fursa na pale inapotokea pande hizi mbili kukutana basi kuna kitu kitatokea. Hebu sasa tutafakari fursa chache ili makala hii iweze kwa na uzito zaidi.

Fursa Ya Maisha

Fursa ya kwanza ni ile hali ya sisi kuendelea kuwa hai, hii ni fursa muhimu ambayo watu wengi wanashindwa kuitambua kila wanapofanya tathmini ya fursa katika maisha. Kwa kitendo tu cha kuwa hai unapaswa kumshukuru Mungu kwani fursa hii ndiyo inayosababisha wewe hata kuona uhitaji na kufikiri.

Unakumbuka ile kanuni ya sumaku? Kwamba ina ncha mbili ncha moja inaitwa S na ncha ya pili inaitwa N. Ili sumaku na sumaku ziweze kuvutana ni pale pande mbili zisizofanana zitakapokaribiana.S na N zikikaribiana basi sumaku huvutana na pale pande zinazofanana zinapokaribiana basi hapo zinasukumana na hazitakaa zikutane hata siku moja mpaka kanuni itakapozingatiwa.

Ukiangalia harakaharaka ungeweza kujaribiwa kuhoji kwa nini S na S au N na N,yaani pande zinazofanana zisivutane? Sasa hiyo ni kanuni na kanuni huwa kama namna fulani ya sheria huwezi kuihoji wala kuibadili ukweli ndivyo ulivyo na unabaki kuwa hivyo.

Maeneo mbalimbali ya maisha ya mwanadamu yanapaswa kuongozwa na kanuni na kama ni kanuni basi huwa kama sheria hazibadiliki. Uwe unajua au hujui kanuni zinabaki kuwa ni kanuni tu. Zipo kanuni za mafanikio katika maeneo mbalimbali na mtu akiwa na taarifa akazingatia na kuzifuata, basi mtu huyo huwa rahisi kufika anakotaka.

Fursa ziko kila mahali na hazijawahi kupunguwa kama ilivyo hewa tunayovuta bila kwisha wala kukatika,tunatembea nazo kila tunakokwenda,tukilala na kuamka tunaamka nazo,katika mazingira yote,hali zote tunaandamana na fursa.

Hebu tumalizie kwa kujibu swali lililoachwa na kichwa cha makala yetu kama “fursa siyo tatizo” tatizo ni nini basi? Tatizo kubwa linalokabili watu wengi ni kutokuwa na macho ya kuona fursa zilipo. Kama ilivyo kwa kanuni ya sumaku mara nyingi mitazamo yetu imepelekea tupishane na fursa.

Fursa zimejaa kila mahali zinatafuta watu wa kuzichukua,ila cha ajabu watu wanaotafuta fursa kila siku wanapishana nazo kwa sababu hawana macho ya kuziona na mwisho wa siku zipo zimekaa tu,kwa kuwa wanakozitafuta siko zinakopatikana. Maisha ni fursa bila mipaka, fursa halijawahi kuwa tatizo ila tatizo ni macho yanayoweza kuona hizo fursa zilipo.

Ndio maana pale unapokaa na kukiri maisha ni magumu,kuna wengine wanamshukuru Mungu kwa kuwa hawajawahi kukutana na fursa ya mafanikio kama wanayokutana nayo wakati huo unaolalamika wewe.Wakati wa vita kuna wanaoumia na wanaonufaika,wakati wa njaa kuna wanaoathirika na wanaonufaika na hiyo hali.

Nataka nikupe kanuni ambayo mimi imenisaidia sana katika maisha yangu.Popote utakapokuwa,chochote utakachokutana nacho,changamoto yoyote utakayokutana nayo,hali yoyote utakayokuwa umekabiliana nayo hakikisha unaipa nafsi yako haki ya kujiuliza maswali mawili muhimu ambayo mimi nayaita maswali ya nguvu. Kuna somo gani ambalo naweza kujifunza kupitia kipindi hiki ninachopita? Pili jiulize kuna fursa gani katika hali hii? Hakuna changamoto ambayo mtu atapita halafu ikamuacha akiwa bila mabadiliko. Changamoto huwa ni fursa ya kutusaidia kuwa watu bora zaidi ingawa katika hali ya kawaida akili hujisukuma kukataa.

Naamini utakuwa umepata kitu kingine leo kupitia makala hii fupi.Kama utakuwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha yako usisite kuwasiliana kupitia njia za mawasiliano hapo chini;aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno,au whatsap au kupiga simu kwa namba hapo chini.
Ni mimi rafiki na kocha Philipo Lulale

WhatsApp: +255784503076                                                      

maishanifursa2017@gmail.com

Previous
Previous

Ulishinda Kabla Ya Kuzaliwa

Next
Next

 Jinsi Ya Kujiongeza Thamani