Alianza Kinyonge Akamaliza kwa Ushindi!

Je umeshindwa mara ngapi katika maisha yako? Jamaa alishindwa kuuza bidhaa yake ya kuku wa kukaanga mara 1009, alikuwa ni mtu ambaye hajawahi kufurahia maisha hata kidogo. Alipojaribu kuuza mapishi yake ya kuku kwa mikahawa na wafanyabiashara, wengi walimkataa, lakini hakukata tamaa. Hatimaye, alifanikiwa kuanzisha biashara yake ambayo sasa ni moja ya mifumo mikubwa ya chakula cha haraka duniani.

Alikuwa na tabia za ajabu zisizokubalika na watu wengi katika jamii. Alikuja kufikia mafanikio baada ya kushindwa mara nyingi. Alishindwa kazi ya kuuza mgahawa,alishindwa kazi ya uanasheria,alishindwa kazi ya uwakala wa bima,alishindwa kuwa na ndoa nzuri. Alijaribu kujiua baada ya kupokea kiinua mgongo kidogo sana ambacho hakuona kama kitamsaidia chochote. Mara nyingi alifanya maamuzi bila busara na alikuwa na tabia ya kupigana kazini hali iliyomgharimu kufukuzwa kazi mara kwa mara.  

Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu katika maisha ya ujana wake wote na utu uzima bila mafanikio.Alistafu akiwa na umri wa miaka 65 kwa mujibu wa sheria na kupata kiinua mgongo chake cha dola 109 za kimarekani hakujua cha kufanya. Hakuona mwanga hata kidogo. Nyuma na mbele ilikuwa giza,kulia na kushoto ilikuwa giza,giza giza giza kila mahali.Alikata tamaa kabisa na suluhu ya hali hiyo akachukua uamuzi wa kujiua lakini hakufanikiwa kutimiza azma yake hiyo ovu.

Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu na kujiuliza nini ambacho angeweza kufanya,alibadilisha mtazamo na kuanza kujiongeze thamani kwanza.Kumbe alikuwa ni mtaalam mzuri sana wa kuandaa kuku wa kukaanga,kazi ambayo aliifanya kwa miaka mingi ingawa hakufanikiwa.Alianza kuiona ile dola 109 kama inatosha kufanya mtaji wa kuku wa kukaanga na kuwauza kwa watu mbalimbali.

Ndipo sasa akanunua kuku wachache   na kuwaandaa kwa ustadi mkubwa na kwenda mlango hata mlango kutafuta soko. Mambo hayakuwa mezuri mapema lakini hakujaribiwa kukua tamaa,badala yake alisukuma bila kuchoka. Bidhaa yake ya kuku wa kukaanga ilikataliwa mara 1009 kabla ya kukubalika katika soko lakini hakukata tamaa.

Katika umri wa miaka 65 mambo yalimnyookea kampuni yake KFC ikawa maarufu sana nchini Marekani na akatengeneza fedha nyingi. Alikuwa na mawakala wa bidhaa yake kila mahali na akawa ni miongoni mwa watu matajiri wakati wake.

Huyu si mwingine ni Mmarekani Colonel Sanders aliyepitia mitihani mingi kabla ya kufikia mafanikio.Alizaliwa mwaka 1890 na kufa mwaka 1980.Mwaka 1964 kampuni yake ilikuwa na thamani ya dola 2 milioni na wakati anakufa alikuwa ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 3.5. Mara nyingi watu tumetumia msemo wa majaribu ni mtaji lakini ni watu wachache wanaoamini katika msemo huo ingawa wanautumia mara kwa mara.

Watu wanaoishi kwa kusudi na maono makubwa wanatazama majaribu kama ufunguo wa mafanikio na ngazi ya kupandia.Wakati wengine wanakata tamaa na kubaki wakilalamika basi palipo na jaribu pana ushindi na kama pana ushindi basi pana mlango wa fursa. Ni jaribu gani unalopitia ambalo unaliona kama mlima mkubwa usioweza kuuvuka? Omba upate macho ya ndani kuona kitu cha thamani kilicho nyuma ya jaribu unalopitia.

Watu wengi wanapenda kuelezea wenzao jinsi walivyofikia mafanikio,kitu kizuri kabisa.Ngoja nikwambie watu wengi wanatamani kusikia milima na mabonde uliyopanda na kushuka.Umeshindwa mara ngapi na ni njia gani uliyotumia kujikwamua mahali ulipokuwa umekwama.jaribu utaniambia.

Kila hali unayopitia tafakari na kujiuliza kuna somo gani ambalo naweza kujifunza kupitia hali hii ninayopitia na nifanye nini ili kuboresha Zaidi? Unaona nini unapopata fursa ya kupitia katika mitihani na majaribu makubwa maishani? Unaona giza tupu au unaona kuna mwanga? Unaona mwanzo wa safari nyingine ya mafanikio au unaona kama ndio mwisho wa dunia yako?

“Amini,Ota,jaribu.Utafikia mafanikio hakuna kisingizio cha umri,kwani umri sio kigezo cha ushindi.

Naamini kuna kitu utakuwa umejifunza cha kukutia moyo kupitia Makala hii fupi.Iwapo ungependa kupata ushauri katika eneo lolote la maisha au kuingia ndani Zaidi ya mada hizi,basi usisite kutuma ujumbe mfupi wa simu,au whatsap au hata kupiga kwa nambari ya mawasiliano hapo chini.

Ni mimi mtumishi wako na kocha:
WhatsApp +255784503076
Barua Pepe: maishanifursa2017@gmail.com

Previous
Previous

Hakuna Jambo Lisilowezekana

Next
Next

Pesa Siyo Msingi Pekee wa Mafanikio