Badili Uchungu Kuwa Wito

Marry Johnson na Oshea Israel

Umewahi kumsamehe mtu aliyekukosea bila kuangalia ukubwa wa kosa alilokufanyia hata kama anaendelea kukukosea?. Mwezi wa pili mwaka 1993 Marry Johnson alipokuwa kazini alipokea simu yenye taarifa mbaya ikimjulisha kuhusu kifo cha mwanaye wa pekee Laramiun Bry ambaye alikuwa ameuawa kikatiri na muuaji Oshea Israel  huko nchini Marekani.

Marry Johnson alitembea na uchungu kwa miaka 12 hata baada ya mkatishaji wa maisha na ndoto za mwanae kufungwa jela miaka 25  alimchukulia Oshea kama mnyama katiri ambaye hakustahili kabisa kupata msamaha na huruma ya aina yoyote ya binadamu wengine kwani dhambi aliyofanya haikustahili kabisa msamaha.

Karibu tena katika makala zetu za kujenga katika mtandao wetu. Kwanza nikushukuru sana kwa kuendelea kutuamini na kufuatilia kazi zetu. Kazi hii ina maana tu kwa sababu wewe upo. Kama ni mara yako ya kwanza kusoma makala zetu nikukaribishe kwa mikono miwili na kuahidi kuwa hutakaa ujute kuufahamu mtandao huu.

Kwa bahati mbaya kadiri alivyoendelea kushikilia jambo na kutunza uchungu moyoni mwake hakuwahi hata siku moja kupata amani wala furaha zaidi ya afya yake kuemdelea kudhoofika kutokana na uamuzi wake wa kutunza uchungu moyoni bila kufikiria madhara yake.

Baada ya kusoma shairi moja lililombadilisha kabisa mtazamo wake alichagua kumsamehe na kwenda kumwona Oshea gerezani kwa ajili ya kumtangazia msamaha na ndipo sasa moyoni mwake alipobaini kuwa kumbe angeweza kubadilisha uchungu kuwa huduma ya kusaidia binadamu wengune  wanaopita katika kipindi kama chake.

“Ghafla nilipata maono kuanzisha shirika siyo tu kusaidia wamama ambao watoto wao wameuawa lakini hata wamama wenye watoto waliopoteza maisha. Nilijua singeweza kusaidia wamama wa namna hii kama kweli nilikuwa sijamsamehe Oshea. Kwa hiyo niliomba kibali kwenye kitengo cha marekebisho ili kukutana naye” ananukuliwa Marry kutoka mtandao wa upworthy.com

Halikuwa jambo rahisi hata Oshea mwenyewe kwa mara ya kwanza alikataa kata kata kukutana na mama wa kijana aliyemuua kwani hakumwamini kabisa kutokana na ukweli kwamba alijaribu mara kadhaa kumwita mama huyo aje gerezani kumpa nafasi ya kuomba msamaha lakini Marry alikataa kata kata kukutana na mtu ambaye mwanzo alimchukulia kama mnyama katiri.

Siku ilipofika Marry na Oshea walikutana pale gerezani alipokuwa anaendela kutumikia kifungo chake wakakumbatiana na kuomba msamaha huku akimtangazia msamaha na kumwambia kwa mara ya kwanza kuwa anampenda jambo ambalo halikutarajiwa kabisa.

Kitendo hicho kilileta uponyaji mkubwa na amani ndani ya moyo na maisha ya Marry kwa ujumla,kuanzia wakati huo alimchukulia Oshea kama binadamu anaestahili kusaidiwa ili kurejea katika maisha ya kawaida hivyo hakuacha kwenda kumtembelea mara kwa mara gerezani.

Miaka 7 baada ya kutangaziana msamaha Oshea alimaliza kifungo chake na aliporudi uraiani alikuwa hana mahali popote pa kwenda Marry Johnson alimchukua na kumtunza nyumbani kwake kabla ya kuanza kuishi naye katika nyumba ghorofa moja ambayo milango yao ilikuwa jirani.

Marry alijisikia kama amempata mtoto wa kiroho ambaye alikuja kuwa mbadala wa mwanaye wa kimwili na Oshea alimchukulia kama mama yake ambaye waliishi kwa ushuhuda na upendo mkubwa.

“Tarehe 12 February 1993 mtoto pekee wa Marry Johnson, Laramium Byrd (20) aliuawa huku muuaji Oshea Israel (16) alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela baada ya kupatikana na hatia ya mauaji. Miaka mingi baadaye Marry alimtembelea Oshea gerezani na tangu alipoachiwa huru mwaka 2010 wameishi kama majirani huko Northside community Minneapolis nchini Marekani” mwisho wa nukuu.

Marry aliamua kuanzisha shirika linalojulikana kwa jina la “From Dearth To Life” ambalo linalenga kuwasaidia watu wanaopitia kipindi kama alichopitia yeye kuwasaidia maisha yaweze kuendelea kama kawaida na Oshea alikuja kuwa mtu wa msaada mkubwa sana kwake kwani walipita kila mahali wakitoa ushuhuda ambao umesaidia watu wengi kupona.

Msamaha kwa mtu anayeamini si jambo la kuchagua ni lazima kufanya kwani ndivyo Mungu anavyotaka tufanye huku tukitanguliwa na upendo katika kila lile tunaloona kuwa ni mapito makubwa.Ukiwa na upendo kusamehe na kusahau ni jambo la lazima.

Watu wengi wameshindwa kuendelea mbele kutokana na kushindwa tu kuachilia uchungu katika mioyo yao wakidhani wanajisaidia kumbe wanajiangamiza na kuwa katika hatari ya kukosa maisha ya duniani na mbinguni pia. Biblia haisemi tusamehe makosa mepesi tu hapana samehe aliyekukosea hata kama anaendelea kukukosea tena usisubiri kuombwa msamaha. 1Kor. 13:4-5.

Kusamehe ni kwa ajili ya wewe mwenyewe unayesamehe wala si kwa ajili ya yule unayemsamehe.Ukikutana na hali ya namna hii au inayofanana na hii uwe mwangalifu uko jirani kubaini wito mkubwa ulio ndani mwako ambao unaweza kuubadilisha uchungu kuwa wito kuhudumia watu wengine kwani dunia inasubiri.
Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala kitu kingine kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha yako usisite kuwasili nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo.

Ni mimi rafiki na kocha Philipo Lulale

Barua Pepel: maishanifursa2017@gmail.com
WhatsApp:+255784503076                                

Previous
Previous

Tofauti Ya Kazi Na Wito

Next
Next

Ujinga Siyo Kitu Kibaya tu!